Hello karibu
katika darasa huru, asante kwa kutembelea blog yetu. Asante kwa mnaoendelea
kutuma maswali yenu, kiukweli tunapokea maswali mengi sana kwahiyo ukiona swali
lako halijajibiwa usidhani tumelidharau au tumelisahau, tunaendelea kuyafanyia
kazi na mtapata majibu hapahapa darasani. Pia kama una swali maoni au ushauri
nitumie kwa email yangu:obbymjuzi@gmail.com.
Leo katika
DARASA HURU tutajifunza jinsi ya kutuma mafile au mafolder ambayo sio audio au
video kwa kutumia whatsaap. Hii itakuwa msaada kwa wale miokuwa mnatamani
kutumiana softwares au notes au documents mbalimbali kwa njia ya whatsaap.
KARIBU
Whatsapp ni app ambayo imekuwa ikitumika na watu wengi
kweny kutuma na kupokea audio na video, ni app inayopendwa na watu wengi sana
kutokana na urahisi wake wa kutumia. Pamoja na kukuwezesha kushare files za
multimedia(music, photos, video) lakini kuna kasoro iliyopo katika app hii.
Nayo ni kwamba Haina uwezo wa kutuma files zilizopo katika mfumo wa software
kama .exe, .apk, .bar n.k na pia files katika mfumo wa document (.docx, .pptx,
.epub). Zipo njia baadhi zinazokuwezesha kutuma na kupokea mafaili ya mfumo
huo, moja ya njia ambayo nadhani inafaa zaidi ni kwa kutumia programu ya
kando(third party app) inayoitwa WhatsApp File Sender.
Kupitia WhatsApp File Sender unaweza kutuma mafaili
kama hati za kiofisi(office documents) (.doc, .docx, pptx), pdf, .epub na
kadhalika. Si hayo tu, kwa kifupi unaweza kutuma na kupokea kila aina ya faili
kwa WhatsApp kupitia programu hii, hata programu kama .exe (executable), .zip
na .apk au chochote kile unachotaka.
JINSI YA KUTUMA FILES
STEPS.
1.Nenda kweny playstore
na udownload Whatsapp File Sender
2. Fungua WhatsApp File
Sender, kisha angalia sehem wameandika SELECT
FILE au chagua mafile utakayayaona chini ya
hio neon SELECT FILE.
3. Tafuta faili
unalotaka kutuma, kisha SEND
4. itakupeleka kwenye whatsapp
account yako
5. Chagua unaemtumia
kisha bonyeza "OK".
NAMNA YA KUPOKEA FAILI
STEPS
1. Download faili kwa WhatsApp yako ya kawaida
1. Download faili kwa WhatsApp yako ya kawaida
2. Baada tu ya kudownload,
WhatsApp File Sender itafunguka yenyewe na kuomba ruhusa yako ili kufungua
faili hilo (decode).
3. Elekeza sehemu unayotaka
kuhifadhi hilo faili, unaweza tengeneza folder lake maalum kwa ajli tu ya
kupokea mafaili kwa njia hii.
4. Kisha bonyeza Ok.
Ili kufanikisha swala
hili ni Lazima wote (mtumaji & mpokeaji ) wawe na WHATSAPP FILE SENDER
(WTS)
WhatsApp File Sender
hubadili mafaili (encoding) kwenda kwenye mfumo wa sauti (audio), na wakati wa
kupokea hurudisha katika mfumo wake
wa kawaida (decoding).
wa kawaida (decoding).
Kwa Kawaida WhatsApp
hutuma faili lisilozidi ukubwa wa MB 16, lakini kwa njia hii unaweza
kutuma faili lenye ukubwa wowote zaidi ya MB16.
kutuma faili lenye ukubwa wowote zaidi ya MB16.
Unaweza tuma vitu vingi kwa mara
moja, tengeneza folder la ".zip" weka mafaili yote ndani yake, kisha
tuma.
WhatsApp File Sender hugawa
mafaili makubwa katika ukubwa wa MB 16 kila moja, hii
huwezesha kutuma mafaili makubwa zaidi.
huwezesha kutuma mafaili makubwa zaidi.
Mpokeaji ni lazima ahakikishe
vipande vyote vimefanikiwa kuwa downloaded kabla ya
decoding.
decoding.
Hii ni Njia nzuri kwa makundi ya
WhatsApp kutumiana mafaili ya kiofisi kama notes na mengineyo kwa urahisi
zaidi.
obby mjuzi & blessed genius